TAIFA KUOMBEWA TAREHE 31 DECEMBER NDANI YA UWANJA WA UHURU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAIFA KUOMBEWA TAREHE 31 DECEMBER NDANI YA UWANJA WA UHURU

 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha  Mkubwa – Dua maalum kwa Taifa  askofu Godfrey Emmmanuel Malasi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkesha mkubwa wa kuliombea taifa utakaofanyika katika uwanja wa taifa  Desemba 31,2011 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete. Wengine ni Viongozi wa kamati hiyo kutoka Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania Christian Fellowship of Churches).
 Viongozi wa mkesha mkubwa wa kuliombea taifa (waliosimama mbele) wakifanya maombi maalum kwa waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuitumikia jamii kwa uadilifu kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.Maombi hayo yamefanyika  leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa  kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru  na kuanza kipindi kingine  ambapo mgeni rasmi  katika mkesha huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania  katika kipindi hiki ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na  kuanza kipindi kingine na kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika uchumi wa taifa.
Amesema serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha  wananchi rasilimali ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili”
Amesema  mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania  ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na  visiwa vya   Zanzbar na Pemba.
Amefafanua  kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa  tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki mkesha huo.
Kuhusu  maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema  yanaendelea vizuri na  kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo maalum na kuongeza  kuwa  mkesha huo utaambatana   na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa  Askofu Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa  ni ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania na watu wake  katika kuheshimu utu na  utamaduni wa taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue athari za dhambi hiyo.
“Sisi kama viongozi wa makanisa katika nchi hii tunapinga kwa nguzu zote vitendo vya ushoga ndani ya taifa letu, vitendo vya ushoga ndivyo vilivyosababisha Sodoma na Gomora kuchomwa moto kwa kuwa vilimchukiza sana Mungu, Sisi kama viongozi wa dini katika kizazi chetu na vizazi vijavyo hatutaki kufikia hapo na kuona taifa letu likichomwa moto”
Na Aron Msigwa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages