Tahadhari kwa Watanzania waishio China hasa Wuhan - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Tahadhari kwa Watanzania waishio China hasa Wuhan

Hii ni tahadhari iliyotolewa na watu wanaoishi maeneo ya Wuhan kuwataka Watanzania popote walipo nchini China hasa kwenye mji wa Wuhan kuchukua hadhari za lazima ili kuepuka hatari.  

Shukran kwa "Mzalendo" aliyeona vyema kusambaza ujumbe huu muhimu.


Wakuu kipindi tunaelekea mwisho wa mwaka kuna matukio mengi mno yanatokea hapa Uchina hususan Wuhan, ingawa kwa wengi wetu tunaweza kudhani kuwa Uchina hakuna uporaji, maharamia n.k.;  Si kweli ila ni kutokana na mazingira ambayo tunaishi hatujawa "exposed" sana kuweza kujua haya mambo, ila ukweli ni kuwa China kuna kila ushenzi kama mahali popote pale duniani. 

Katika siku hizi za karibuni kwa wale wafuatiliaji mtakuwa mmejionea matukio kadhaa, mfano:

  1. Utekaji wa watu na kutoa viungo vya ndani (this happened in many Chinese Cities, Wuhan is one of them)
  2. Upigaji wa bomu kwenye benki ya Communication iliyo karibu na Zhongshan Middle School ili kupora fedha. Tukio lililopelekea watu kadhaa kujeruhiwa na mmoja kupoteza maisha palepale.
  3. Jana mchana, benki nyingine Mishen Bank Donghu Branch ilivamiwa kwa mtindo huo huo.
  4. Wiki mbili zilizopita jamaa walifunga mtaa shuleni kwetu mitaa ya saa sita usiku na kusabababisha kizaazaa.
  5. Binafsi niliibiwa kadi ya benki nikiwa nalipia dawa. Ilikuwa hospitalini. Kitendo kilikuwa kama mazingaombwe kwani ndani ya sekunde kadhaa (ninamaanisha SEKUNDE kweli) kadi niliyotumia kulipia dawa sikuiona wakati Hospitali hakukuwa na watu wengi (was one of the private Hospital.)

Hayo ni yale ambayo tumeyasikia au kuyashuhudia, kwa wale wanaojichanganya na Wachina watakuwa tayari washataarifiwa hilo kwani siku hizi hii ni mada moto. 

Sasa binafsi ninakushauri yafuatayo:

  1. Punguza nyendo za usiku zisizo na tija, haswa kwa wale wenzetu ambao kila wakati wapo "tilalila". Watu WANATAKA VIUNGO jamani. Inapobidi omba "kampani" ya watu wengine.
  2. Usiende sehemu usiyoijua na Mchina usiyemuamini au asiyeaminika.
  3. Usichukue mula usiku labda iwe ni dharura isiyosubiri, na inapobidi basi tafuta benki zilizo wazi.
  4. Epuka mikwazo na Wachina ikiwemo kugombea wachumba, kwani hasira kwenye jambo A linaweza kuwa ni  kichocheo kwa tukio B (mnajua ninamanisha nini hapa).
  5. Epuka "Ganbei" (mitoko) ya ajabu na Wachina. Hii haswa kwa wale wanaojiachia kwani wanaweza tumia vilevi kukuzimisha au kukuwekea kitu.

Niishie hapa, haya niliyoyasema ni kwa ajili ya usalama wa wote na ni maono binafsi. Mnakumbuka tukio lililomtokea jamaa wa Rwanda (Burundi) mwaka jana. Shime mjilinde!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages