Balozi Mwanaidi Maajar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi Hassan Maajar Trust
akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua
madawati katika shule mbalimbali nchini iliyoandaliwa na taasisi hiyo,
hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu, na
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu wa serikali pamoja na
baadhi ya mawaziri na wakuu wa makampuni mbalimbali jijini Dar es
salaam. Kauli mbiu ya hafla hiyo ni A Desk For Every Child.
Waziri
Mkuu mstaafu Fredirick Sumaye akisalimiana na Balozi Mawaidi Maajar
wakati Mh. Sumaye alipowasili ukumbini hapo, kulia ni Mama Esther
Sumaye.
Waziri
Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba kulia akiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serenget SBL
Mzee Mark Bomani.
Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo usiku huu. 





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)