WAKATI
jumla ya sh. Milioni 55 zimechangishwa katika maonyesho ya mitindo kwa
ajili ya kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa UKIMWI duniani (Red
Ribbon Fashion Gala), mwanamuziki nyota nchini, Diamond aling’ara
vilivyo kwa kuonyesha kipaji kingine cha maonyesho ya mavazi.
Fedha
hizo zilipatikana kwa njia ya mnada wa vitu mbali mbali na nyingine
zikitolewa kwa njia ya udhamini wa shughuli hiyo iliyotumika pia
kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa Ukimwi Duniani.
Mwanamboka
alisema kuwa kituo hicho kitajengwa jijini na kitatoa mafunzo ya njia
mbali mbali za kupambana na maisha, Ujasiliamali, Ushonaji nguo, mafunzo
ya kompyuta na jinsi ya ubinifu wa mitindo au mavazi.
Alisema kuwa jumla ya watoto yatima 100 watakuwa wanapata mafunzo katika kituo hicho kila mwaka.
Baadhi
ya wadhamini waliochangia kufanikisha kwa fedha hizo ni kampuni ya simu
ya mkononi, Vodacom Tanzania na wadau wa maonyesho ya mavazi ambao
walichangia kimya kimya katika maonyesho hayo yaliyofanyika kwenye hotel
ya Double Tree.
Katika
maonyesho hayo, mkali wa miondoko ya Bongo Fleva nchini, Diamond naye
alifanya vitu vyake jukwaani kwa kuvaa nguo aina ya Kidoti iliyobuniwa
na mbunifu chipukizi, Jokate Mwegelo.
Wengine
walioonyesha mavazi jukwani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark
Production, Ritha Poulsen ambaye baadaye nguo yake iliunuliwa na mcheza
filamu maarufu nchini, Steven Kanumba.
Wadhamini
wengine wa shughuli iyo walikuwa Redds, Clouds Entertainment, Kiondo
Communications, I_View Media team na Hall Neel Production. Wengine
waliosaidia maonyesho hayo ya mavazi ni Amaya Beauty Saloon and SPA,
Bank M Tanzaniia, Stanbic Bank, Mimis collections, Kidoti By Jokate
Mwegelo, Bongo Real Mamaz na Bluecherriemoe.
Wadau
wengine ni Flaviana Matata Foundation, Amina Design, Jenifa Pemba, FM
Express events and services ltd, Ernst &Young, ,LR Creations, Millen
Magese Foundation Tiffex, Cool Blue Iku Lazaro, Miraj Kikwete, Halima
Kamus, Mabibo Beer Wines nd Spirits Ltd, and World Link Travel and Tours
ltd.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)