SAFARI YA KUPANDISHA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO YAANZA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SAFARI YA KUPANDISHA MWENGE WA UHURU MLIMA KILIMANJARO YAANZA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas Gama pamoja na Viongozi wa Mkaoa wa Kilimanjaro na wawakilishi wa Wizara ya Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo wakiwasindikizaVijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro tayari kwa safari leo Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro. 

Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wanaonekana wakianza safari yao kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro Marangu Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Leonidas Gama akimpa mkono wa kumtakia heri mmoja wa vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro zilizoko Marangu Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011.
 
Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro walioagwa rasmi na Mhe.Rais Jakaya Mrisho Kikwete Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam hivi karibuni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Leonidas T. Gama akiwaaga kwenye shughuli fupi iliyofanyika Marangu kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011
Vijana wanaopandisha Mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa tayari kwa kuanzakupandisha mlima huo na Mwenge.
watoto wakiangalia shughuli ya kuwaaga wanaopandisha mwenge kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwenye Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Marangu Mkoani Kilimanjaro leo tarehe 5.12.2011. Picha na Anna Itenda -Maelezo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages