Na Mwandishi Wetu
MABONDIA
Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’
wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika
pambano lisilo la ubingwa.
Pambano
hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika
kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .
Siku
kumi kabla ya mpambano mabondia Rashid Matumla na Maneno Osward
walishauriana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya
kuongeza nguvu kama wanatumia na wameshapimwa na Daktari wa mchezo wa
ngumi nchini Charles Kilaga, sheria za mchezo huo haziruhusu kutumia
dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Hivyo mabondia wote wamekutwa wapo fiti na wanatarajia kuzipiga jumapili ya tarehe 25
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'Mwayamwaya' ambaye ndiye
muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili
kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho
Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa
hawakumtendea haki wakati walishawahi kupigana mara mbili nyuma ambapo
Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kushinda mara
moja.inachukuliwa kwamba mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina
yao.
Mpambano
huo Utasindikizwa na mabondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa
Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga
atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa
mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa
mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za
masumbwi.
Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo
yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa
pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.
'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd
Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja Mtagwa
anayefanya shughuli zake Marekani.
DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa
kujua sheria na mafunzo ya ngumi, DVD hizo zinafundisha mambo mengi ''
alisema Super D.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)