BARCELONA YATWAA KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BARCELONA YATWAA KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI LEO


Lionel Messi akishangilia na mchezaji mwenzake, Daniel Alves (2) baada ya kuifungia timu yake bao dhidi ya Santos katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyopigwa Yokohama, Japan leo. Barcelona imeshinda bao 4-0.

Cesc Fabregas akiifungia Barcelona bao la tatu dhidi ya Santos katika fainali ya Klabu Bingwa Duniani iliyopigwa Yokohama, Japan leo. Barcelona imeshinda bao 4-0.
 
TIMU ya Barcelona ya nchini Hispania leo imetwaa tena Kombe la Klabu Bingwa Duniani baada ya kuilaza Santos ya Brazil kwa mabao 4-0.  Barcelona wamechukua kombe hilo kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu baada ya kulinyakua mwaka 2009.


Magoli ya Barca yamewekwa kimiani na Lionel Messi  dk ya 17 na 82, Xavi dk ya 24, na Cesc Fabregas dk ya 45.Picha Zote na Yahoo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages