Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Afanya Ziara Katika Vyanzo Vya Maji Mjini Magharibi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Afanya Ziara Katika Vyanzo Vya Maji Mjini Magharibi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya maji( ZAWA), DK MUSTAFA ALI GARU,alipofanya ziara ya kutembelea Vianzio vya maji katika matangi ya Saateni Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya maji( ZAWA), DK MUSTAFA ALI GARU,(kushoto) pamoja na wataalam wa maji alipofanya ziara ya kutembelea Vianzio vya maji katika matangi ya Welezo, Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,pamoja na viongozi wa ZAWA katika ziara maalum ya kutembelea Vianzio vya maji katika chemchem ya maji Mwanyanya nje ya Mji wa Zanzibar leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiangalia chem chem ya maji Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi akifuatana na viongozi wa mamlaka ya maji ZAWA leo, alipofanya ziara ya kutembelea Vianzio vya maji katika Mkoa wa huo.Picha na Ramadhan Othman,ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages