Mkuu
wa Mkoa Singida Dk.Parseko Kone, kwa niaba ya Rais Dk.Jakaya Kikwete,
akikabidhi zawadi ikiwemo mchele na mbuzi wawili kwa ajili ya kituo cha
Malezi Kititimo kilichopo mjini Singida, kwa ajili ya watoto hao
kusherehekea vizuri sikukuu ya Krismasi,Watoto hao wanaishi mazingira
hatarishi, wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya Singida Paschal Mabiti
na kulia kabisa ni kaimu mkurugenzi manispaa Singida, Simon Hoja.
Singida,Desemba 23,2011.
RAIS
Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya sikukuu ya Krismasi, kwa ajili ya
watoto wanaolelewa na kituo cha Malezi Kititimo, kilichopo Mjini
Singida.
Zawadi
hiyo ya Krismasi kwa kituo hicho, imetolewa jana ijumaa, na Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone, kwa niaba ya Rais Dk.Jakaya Kikwete.
Akikabidhi
zawadi hizo, Rais Dk.Kikwete amewatakia kila la heri watoto hao, katika
kusherehekea sikukuu hiyo, na anawaomba wajione sawa na watoto wengine
duniani katika Krismasi hiyo.
Msaada
huo wa chakula uliotolewa ni mchele kilo 60, mafuta ya kupikia dumu
moja kubwa, mbuzi wawili na viungo mbalimbali kwa ajili ya mapishi,vyote
vikiwa na thamani ya Sh.550,000.
Mkuu
wa mkoa Singida, Dk.Kone, naye aliunga mkono msaada huo kwa kutoa
katoni moja ya juisi, boksi moja la biskuti na mifuko ya pipi.
Wakitoa
shukrani hiyo, watoto hao walimshukuru Rais Kikwete kwa kuwakumbuka
kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)