MAHAFALI YA SABA YA CHUO KIKUU CHA SUZA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAHAFALI YA SABA YA CHUO KIKUU CHA SUZA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho hawapo pichani kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Shahada ya Udaktari wa  Heshima wa Falsafa Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Zanzibar Dk.Aman Abeid Karume katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUZA pamoja na wahitimu wa Chuo ngazi ya Stashahada baada ya kuwatunuku Stashahada zao katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.PICHA ZOTE NA HAMAD HIJJA-MAELEZO ZANZIBA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages