Rais Joseph Kabila akiwa katika moja ya mkutano
WAKATI Rais
Kabila akitarajia kuapishwa leo Jijini Kinshasa na Mpinzani wake
akipanga kujiapisha mwenyewe wiki ijayo, tayari Jeshi la Congo
limesambaza vifaru na majeshi ya kulinda amani katika maeneo ya jiji
la Kinshasa kama hatua ya kujiandaa na lolote linaloweza kutokea katika
sherehe za kuapishwa kwa Rais Joseph Kabila kufuatia Uchaguzi wenye
utata uliofanywa mwezi uliopita.
Ni
viongozi wachache tu wa mataifa ya Afrika wameahidi kuhudhuria, na
waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ubelgiji aliyekuwa amepanga kuhudhuria
sherehe hizo ameahirisha ziara hiyo, kutokana na dalili zilizokuwapo za
kutokea machafuko.
Ameahidi kuwa huenda akafika nchini humo baada ya matangazo ya uchaguzi wa Bunge kutangazwa katika mazingira yaliyo bora zaidi.
Wachunguzi wa nchini na wa kimataifa wameshutumu ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa upigaji kura katika uchaguzi wa Urais na Bunge uliofanywa Novemba 28; tayari kiongozi mkuu wa upinzani Etienne Tshisekedi amejitangaza kuwa Rais baada ya kukataa kukubali matokeo hayo.
Tshisekedi alisema Jumamosi iliyopita kuwa atajiapisha mwenyewe kuwa Rais baadaye juma hili katika uwanja mkuu wa michezo jijini Kinshasa. Kiongozi huyo wa upinzani pia alitoa wito kwa vikosi vya usalama viheshimu amri yake badala ya Rais Kabila, na kusema kuwa tayari amekwisha vunja Serikali ya Rais Kabila.
Upande wa Rais Kabila umetaja matamshi ya mpinzani huyo,Tshisekedi kuwa ni ya Kihuni.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)