Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Bamaga, Mwenge jijini.
Jamaa huyu anaonekana akilalamika akiwa kwenye foleni hiyo.
Jamaa huyu anaonekana akilalamika akiwa kwenye foleni hiyo.
Baadhi ya madumu ya kuchukulia mafuta yakiwa yamepangwa kwenye foleni na wateja, tayari kwa kutiwa mafuta iwapo yatapati.
Magari yakiwa kwenye msululu wa kugoja kujaziwa mafuta.
SAKATA la kuadimika kwa nishati ya mafuta nchini limeibuka tena leo,
ambapo wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameendelea kuhangaika kutafuta
nishati hiyo bila mafanikio. Tatizo hilo linazidi kuipaka matope Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (Ewura), kufuatia kutoweka wazi tatizo linalosababisha
upatikanaji wa mafuta katika vituo mbalimbali.
Baadhi ya wateja wa nishati ya mafuta ya petroli na dizeli leo
wamelalamikia utaratibu wa vituo vya mafuta kuendelea kugoma kuwauzima
nishati hiyo kwa madai ya kwisha katika vituo vyao.
“Inanikela sana hali ni mbaya maana nimetafuta mafuta tangu asubuhi
sijapata, na nikiangalia sababu hata sielewi, nini kinachowafanya Ewura
kutosema tatizo kwetu wateja wao ili tusisumbuke?” alihoji mkazi mmoja
huku mwingine naye akilalamika kuwa:
“ Hawa Ewura hawafai kabisa, yaani leo wamenifanya kutoenda kazini
kwa ajili ya kuhangaika huku na kule kutafuta mafuta, huwezi kuamini,
gari limenizimikia Sinza Mugabe na sasa niko hapa kituo cha mafuta
Bamaga tangu saa tatu asubuhi na mafuta sijapata, wauzaji wanatuyeyusha
tu.” Alisema mkazi huyo.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)