
Rais Kikwete akipokea mwenge wa uhuru kutoka
kwa kiongozi wa mbio hizo mwaka huu

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi mwenge wa
uhuru mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange ambaye atawakabidhi
wapandishaji mlima kilimanjaro

Rais Jakaya Kikwete akiwatakia heri Mkuu wa
Majeshi ya Tanzania Jenerali Davies Mwamunyange na wanajeshi
wataopandisha kilele cha mlima Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru mkesha wa
siku ya uhuru. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt Emmanuel Nchimbi , wa pili kulia ni Naibu waziri katika wizara
hiyo Dkt Fenella Mukangara na wa kwanza kushoto ni mmoja wa
wataopandisha Mwenge mlima Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma
Mwassaakipokea kikombe cha ushindi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete akikabidhi mfano wa hundi
ya shilingi milioni moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwassa na
maafisa wake baada ya mkoa huo kuibuka mshindi wa jumla wa mikoa
iliyofanya vyema katika mbio za mwenge wa wingi wa miradi na maandalizi.

Rais Jakaya Kikwete akihutubia
katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Saidi Mwema,
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge Mh Anne
Makinda

Mama Maria Nyerere na Mama Salma Kikwete na
wageni wengine mashuhuri jukwaa kuu.


Rais
Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya kilele cha mbio za mwenge


Sehemu ya umati wa watu

kikosi cha wataopandisha mwenge wa uhuru mlima
kilimanjaro.Picha Zote na IKULU





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)