Mama Mzazi wa mtoto Jifti Bi. Adela Kakopayani akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kutokea Shinyanga ambapo
mtoto wake atapatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili kwa hisani
ya Precision Air. Kushoto ni Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air Bw.
Tuntufye Mwambusi na Bw. Benson Chuwa Afisa Huduma wa Precision Air
uwanjani Julius Nyerere.
Mtoto Jifti Shomari (2) na hali yake kama
inavyoonekana la tatizo la kuvimba kwa tumbo kutokana na kusumbuliwa na ini.
Anayembeba ni mama yake mzazi Bi. Adela Kakopayani.
Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air Bw.
Tuntufye Mwambusi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuwasili kwa mtoto Jifti na mama yake Adela kutokea Shinyanga kwa hisani ya
Precision Air.
Mama Jifti akitoa maelezo juu ya mtoto wake
mgonjwa Jifti. Pembeni ni Bw. Benson Chuwa Afisa Huduma wa Precision Air
uwanjani Julius Nyerere.
...............................
Shirika la ndege
la Precision Air leo imejitokeza kumsaidia mtoto Jifti Shomari (2) kutokea
Shinyanga anayekabiliwa na ugonjwa wa kuvimba kwa tumbo kutokana na matatizo ya
ini.
Akizungumza katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Meneja Mauzo Taifa wa
Precision Air Bw. Tuntufye Mwambusi alisema kwamba shirika hilo liliguswa sana
na hadithi ya mtoto huyo aliyeelezea mama yake walipoonekana kwa mara ya kwanza
katika vyombo vya habari kama wiki mbili
zilizopita.
“Kama shirika la
ndege la kibiashara tunatambua kwamba tuna wajibu pia kwa jamii na ndo maana katika
moja ya shughuli zetu tumeamua kumsaidia mtoto Jifti kupatiwa matibabu ili naye
siku moja aweze kuwa na faraja ya kuishi na kucheza kama watoto wengine,”
alisema Mwambusi.
“Tunaamini
kwamba usafiri wa ndege wa kwenda na kurudi tuliyoutoa kwa yeye na mama yake mzazi
kutokea Shinyanga kuja Dar imewarahisishia sana kazi kutokana na ukweli wa hali
ya uvimbe wa tumbo lake. Pamoja na hayo, tunaazimia kwamba zawadi ya fedha
taslimu tuliyotoa itasaidia pia katika matibabu yake hospitalini Muhimbili,”
aliongeza Mwambusi alipokuwa uwanjani hapo
kumpokea mtoto Jifti na mama yake.Naye mama yake
mzazi Jifti Bi. Adela Kakopayani alitoa shukurani zake za dhati kwa shirika la
ndege la Precision Air.
“Napenda kusema
ahsante sana kwa shirika hili la ndege la Precision Air kwa kuweza kunifikiria
mimi na mwanangu Jifti. Mungu awabariki na awazidishie kwa moyo huu mzuri wa kujitolea,”
alisema Bi. Kakopoyani.
Wakati huo huo
Meneja Mauzo Taifa wa Precision Air pia alitoa rai kwa makampuni mengine na
watu binafsi kujitokeza pia kumsaidia mtoto huyo.
Mtoto Jifti anatatizo
ya ini inayemsababishia hali ya kuvimba katika tumbo lake. Baada ya kusumbuliwa
na matatizo hayo kwa muda wa mwaka mmoja sasa mama Jifti alishauriwa na
hospitali ya halmshauri na mkoa wa Shinyanga kuja kupatiwa matatibabu
hospitalini Muhimbili ambapo tatizo hilo linaweza tibika.
Mama Jifti
anapatikana kwa nambari ya simu 0786 228 284 kwa wasamaria wema wowote wengine watakayeguswa
kumsaidia mtoto huyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)