Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi
msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik ,
katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi
ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa
na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali
ya mkoa huo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye akizungumza na
kina mama wenye watoto, ambao aliwakuta kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam, leo, alipokwenda kutoa msaada wa CCM wa vyakula kwa
waliopatawa na mafuriko. Kina mama hao, Mariam Msimbi na Asha Selemani
(kulia) walifika kwenye ofisi hiyo kutafuta ufumbyuzi wa ndoa zao
ambapo wamedai wametorokwa na waume zao huku wakiwa na watoto wadogo.
Mape
akizungumza na baadhi ya wananchi alipofika kwenye kambi maalum ya
Mchikichini walikohifadhiwa waathiorika mwa mafuriko, wilayani Ilala.
"Ttunashukuru
serikali imetuhudumia vizuri sisi waathirilka.. wanaolalamika ni wale
wanaojichomeka ili wapate msaada wakati si wahusika.." akisema mmoja wa
wazee (kulia) ambao Nape alizungumza nao kujua serikali ilivyosaidia
waathirika wa mafuriko, alipotembelea kambi la Mchikichini
walikohifadhiwa kwa muda waathirika hao,leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)