Arusha, Desemba 11, 2011. Mashindano
ya gofu ya kitaifa yaliodhaminiwa na Precision Air ikishirikiana na Kenya
Airways yanaendelea vyema katika viwanja vya Gym Khana jijini Arusha.
Akizungumza na
waandishi wa habari Afisa Mawasiliano wa Precisoin Air Amani Nkurlu alisema
mashindano hayo yanayojulikana kwa jina la ‘Chairman’s Trophy’ yameanza tokea
jana na yameweza kukusanya wachezaji 78 kutokea vilabu vya gofu tofauti tofauti
nchini yakiwemo Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Moshi na kadhalika.
“Tumewahi
kudhamini mashindano haya kwa mara kadhaa sasa, na tunapenda kuwahakikishia
wachezaji na washabiki wa gofu kwamba tutaendelea na moyo huu huu wa kuweka
jitihada katika kukuza mchezo huu nchini,” Nkurlu alisema.
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Patrick Ndekana amesema kwamba
shirika hilo limeamua kudhamini mashindano hayo ili kukuuza mchezo huo nchini Tanzania
na kwa lengo la kuvutia vijana na wachezaji chipukizi katika mchezo huo.
“Kuna dhana
potofu kwamba mchezo wa gofu ni kwa ajili ya matajiri na wazee tu, lakini kwa
kupitia mashindano haya tunapenda kuwaelimisha jamii kwamba hata vijana
wanaweza kushiriki ma kuchipukia katika mchezo huu.”
Naye Mwenyekiti
wa Umoja wa Gofu nchini Bw. Paul Matthysen amesema kwamba mashindano hayo
yanaisha jioni ya leo huku wakitegemea washindi katika ngazi ya ‘1st
winner, Longest pin na Nearest pin’ kwa pande zote za wanawake na wanaume.Mashindano haya
ya gofu yameandaliwa na Umoja wa Gofu nchini inayojulikana kama Tanzania Golf
Union (TGU) na yamewezeshwa kupitia makampuni maarufu ya ndege nchini na Afrika,
Precision Air na Kenya Airways.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)