Afisa
Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCAT) Joseph
Kanyunyu akitoa ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan
Mwinyi jana jijini Dar es salaam juu ya miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na Mfuko huo wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la
Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania
Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Sera Wizara ya Fedha Joseph Kiraiya akitoa
ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana
jijini Dar es salaam juu ya mafanikio mbalimbali ambayo Wizara hiyo
imeyapata katika kuwaletea maendeleo wananchi wakati kiongozi huyo
alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya miaka 50
ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kulia) akibadilishana
mawazo jana jijini Dar es salaam na Katibu wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii Blandina Nyoni wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa
Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
Afisa Mauzo wa Benki ya Posta David Philipo akitoa ufafanuzi kwa Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana jijini Dar es salaam
juu ya huduma ya Benki Popote inayotolewa na Benki hiyo wakati kiongozi
huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa maonyesho ya
miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) Mordgard Lumbanga akitoa
ufafanuzi kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alli Hassan Mwinyi jana
jijini Dar es salaam juu ya mafao mbalimbali yatolewayo na mfuko huo wakati
kiongozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye wa
maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi akiangalia kikundi cha
sarakasi cha Mama Afrika kikiwaburudisha wananchi jana jijini Dar es
salaam waliotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati maonyesho ya miaka
50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO_ Dar es salaam




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)