TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwanza,
Desemba 1 2011.
Precision Air-shirika la ndege linaoongoza Tanzania ikishirikiana na Shirika la
Mazingira na Uhifadhi Tanzania (TECO) kwa pamoja wameweza kupanda miti zaidi ya
5000 katika magereza ya Butimba leo jijini Mwanza kama namna ya kuinua uhifadhi
wa mazingira nchini.
Mkurugenzi wa usafirishaji wa mizigo wa Precision
Air Bw. Elias Moshi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, alisema
kwamba wakati Tanzania ikisheherekea miaka 50 ya uhuru sasa, ni vyema
tukawakumbuka na kuwaandalia mazingira bora watanzania wa vizazi vijavyo ili na
wao waweze kufaidi matunda ya nchi yetu huko baadaye.
“Kupanda miti si jukumu la serikali tu
bali ni kwa watanzania wote kwa ujumla. Ndo maana leo kama wafanyakazi wa
Precision Air tumeamua kutoa kipaumbele katika mazingira ili kuwa mfano kwa
wananchi wengine,” aliongeza.
Pia Bw. Moshi alipendekeza serikali
kupitisha mpango maalumu wa kupanda miti na kukagua kama wamiliki mbali mbali
wa ardhi wanafuata hiyo. Akisisitiza kwamba ungekuwa mpango madhubuti ya
kuhifadhi mazingira nchini.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa TECO Bw.
John Masweta alisema kwamba katika miaka 50 ya uhuru ya Tanzania ingependeza
zaidi kama watu watasherehekea kukiwa na uhakika wa mazingira bora pia.
“Kusema tunashehereka miaka 50 ya uhuru tu
peke yake haitoshi, bali ni vizuri tukatafakari kuhusu namna tunavyoathiri
mazingira yetu na tunaweza kufanya nini ili kuweza kuyaboresha,” alisema.
Kwa pamoja Bw. Masweta na Mkurugenzi wa
Precision Air Bw. Moshi waliishukuru utawala wa magereza ya Butimba kwa nafasi
yakipekee waliyopewa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Magereza ya
Butimba Bw. Edson Yalimo alisema ni jambo jema Precision Air walilofanya wakishirikiana
na TECO kuyakumbuka hata mazingira ya watanzania waishio magerezani.
“Tunawashukuru sana kwa kujali kwenu
alisema,”alisema.
Mwisho. Imetolewa na
Ofisi ya Mawasiliano Precision Air: 0786404010/0712223839









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)