NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
MSANII
wa kizazi kipya Abel Motika maarufu Mr Ebo(37) aliyefariki desemba Mosi
mwaka huu saa 4.30, katika hospitali ya misheni(Dream) iliyopo Usa River wilayani Arumeru ,anazikwa leo jumatatu katika shamba la baba yake mzazi eneo la Kijenge chini ,manispaa ya Arusha.
Mazishi
hayo yanatarajiwa kuvuta umati mkubwa wa wakazi wa maeneo mbalimbali
nchini wakiwemo mashuhuri na tayari wageni mbalimbali wameingia
kushiriki mazishi hayo ,ambapo pia wasanii mbalimbali kutoka Mkoani
Tanga,Dar es salaam na mikoa mingine jirani wanataarajiwa kuhudhulia
mazishi hayo.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Mzee Motika
,ambaye ni kaka mkubwa wa marehemu Mr Ebo,Olais Motika(58) alisema kuwa
mazishi hayo yanatanguliwa na misa maalumu ya kuuombea mwili wa
merehemu katika kanisa la Luthelani ,lililopo kata ya Olorien.
Alisema kuwa marehemu Ebo
alikuwa mtoto wa 10 kati ya watoto 11 wa mzee Loshilaa Motika(85)ambapo
kati yao wawili ni marehemu akiwemo Mr Ebo na kwamba marehemu alioa na
kuzaa watoto watatu .
Alisema katika familia yao yeye Olais ni mtoto wa kwanza na kufuatiwa na Sion,John,Michael,Rose( marehemu) Ana,Kesia,Grace ,Imanuel ,Mr Ebo(marehemu) na Jackon ambaye ni mtoto wa mwisho.
Akisimulia
zaidi , alisema kuwa marehemu alianza kuugua maradhi mbalimbali miezi
mitano iliyopita na kutibiwa katika hospitali mbalimbali hapa nchini,
ikiwemo hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro.
Aidha alisema awali marehemu Mr Ebo alikuwa akiishi Kisosora mkoani Tanga na
kufanya shughuli zake mkoani humo baada ya kujenga nyumba yake kubwa na
kufungua studio aliyokuwa akiimiliki na kurekodi nyimbo mbalimbali za
wasanii wa mziki.
Aliongeza
kuwa usanii alianza mwaka 2001 baada ya kutoa nyimbo yake ya ‘mimi
mmasai bana’ hatua ambayo iliwashangaza familia yake lakini akadai
kwamba walifurahia kazi yake kwa kuwa ilichangia kwa kiasi kikubwa
kuitangaza familia ya mzee Motika na kufanya jina la Motika lijulikane .
Alifafanua
kwamba baada ya kuugua na kuzidiwa alilazwa katika hospitali hiyo ya
misheni na kwa mujibu wa waunguzi wa hospitali hiyo walieleza kwamba
hali ya Mr. Ebo Ilikuwa ikibadilika mara kwa mara hadi desemba mosi
majira ya saa 4.30 usiku alipofariki dunia baada ya hali yake kuwa mbaya
zaidi.
Nae baba mzazi wa marehemu Mr Ebo,Mzee Loshinaa alisema
kuwa amesikitishwa sana na kifo cha marehemu mwanae kwa kuwa
hakutegemea kwamba ipo siku mwanae huyo aliyeipaisha familia yao
angemtangulia ,hata hivyo ameiomba jamii kumwombea kwani mungu ametwaa
na jina la bwana lihimidiwe.
Marehemu
Mr Ebo ameacha mke,aliyetajwa kwa jina la Baby Shoo ,watoto watatu
ambao ni Ashrey ,Adella na Alisha na wawili kati yao wanasoma nchini Uganda
na watakuwepo kwenye mazishi ya baba yao ,pia marehemu ameacha vitu
mbalimbali ikiwemo nyumba iliyopo mkoani Tanga na Studio ya kurekodi
mziki.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)