Mtandao
wa Wanataaluma Tanzania umemtunuku nishani maalum Baba wa Taifa, Hayati
Mwalimu Nyerere katika kongamano la wanataaluma hao leo kwenye ukumbi
wa Mlimani City Dar es Salaam. Pichani, Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akikabidhi tuzo hiyo kwa mtoto wa
Malimu, Makongoro Nyerere wakati wa kongamano hilo. Kulia ni Rais wa
Mtandao huo, Phares Magesa.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa
Taifa, hayati Mwalimu Nyerere akimuonyesha tuzo hiyo, Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye. Kulia ni Mbunge wa
Ubungo (CHADEMA) John Mnyika.
"Ukosefu
wa ajira kwa wasomi husababisha baadhi yao kushawishiwa kwa urahisi
kushiriki maandamano" Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
(kushoto) akisema maneno hayo wakazi akizungumza na Mbunge wa Ubungo
(CHADEMA) John Mnyika (kulia), Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Makongoro
Nyerere na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu
wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa
Ubungo (CHADEMA) John Mnyika katika kongamano la Mtandao wa Wanataaluma
Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Katika kongamano hilo Nape na Mnyika wametoa mada 'Uzalendo na Utaifa'.
Makamu
kuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete akijadili jambo
na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Rais
wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania, Phares Magesa, wakati wa kongamano
la wana taaluma hao kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)