Filamu ya Mr President yazinduliwa rasmi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Filamu ya Mr President yazinduliwa rasmi

Vick Kamata, Mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye ndiye Mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Mr. President uliofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam, akiizinduzi filamu hiyo ambayo inaelezea maisha ya kiongozi wa nchi . 
Vick Kamata amewaeleza wasanii mbalimbai waliohudhuria katika uzinduzi huo kuwa anaimani kuwa sheria mpya ya haki miliki itatungwa na Bunge ili kulinda kazi za wasanii kutokana na kuibiwa kazi zao muda mrefu. Ameongeza kwamba kazi ya sanaa ni kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwasaidia wasanii kuishi maisha mazuri, lakini pia kufanya maendeleo katika maisha yao. 

Vick Kamata amezindua filamu hiyo kwa niaba ya Waziri Mathias Chikawe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo hata hivyo hakuhudhuria kutokana na majukumu mengine ya kitaifa
Eddie Hanspoppe mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Papa Zii akizungumza katika uzinduzi huo, ambapo amewashukuru wageni waalikwa wote waliohudhuria katika uzinduzi huo, akisema wameonyesha kwamba wamesikia wito wa kampuni ya Papa Zii, na ameahidi kuwa kampuni hiyo itatekeleza na kusimamia vyema kazi za wasanii hapa nchini.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Papaa Zii Vivian Sirikwa akizungumza katika uzinduzi huo na kuelezea malengo ya kampuni hiyo, katika kukuza sanaa na kuendeleza wasanii hapa nchini.
Steve Mengele aka Steve Nyerere akitambulisha waigizaji wenzake walioshiriki katika filamu ya Mr. President ambayo yeye mwenyewe ameigiza kama Rais katika filamu hiyo, huku waigizaji wenzake wakonekana wenye furaha katikauzinduzi huo.
Wsanii mbalimbali walioshiriki kuigiza filamu ya Mr. President wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Papa Zii Vivian akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam.
Peter John Lugabandana akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi na kukaribisha wageni mbalimbali.
Bendi ya Borabora Sound ikitumbuiza katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam.
Vick Kamata kulia mgeni rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya Mr. President iliyoandaliwa na kampuni ya Papa Zii unaofanyika usiku huu kwenye hoteli Serena Dar es salaam usiku huu, ambapo wageni waalikwa mbalimbali wameweza kufika katika uzinduzi huo ili kushuhudia kitakachojili kwenye uzinduzi huo, katikati ni Mbunge wa Mbinga Magharibi Kpt. John Komba na kulia ni Benny Kinyaiya.
Wazee wa mpira kutoka kulia ni Evans Aveva akiongea na Charles Hamka, Mohamed Nasor, Philemon pamoja na Juma Pinto wakishiriki katika uzinduzi huo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni mtu mzima John Kitime, Rich Mtambalike na wapili kutoka kulia ni Cloud pamoja na marafiki zao.
Richard Mzirai pamoja na Mr Bandawe wakiwa katika uzinduzi huo kama wanavyoonekana.
Wadau Hamatton Bhao kulia na Rupe Mohamed wakishuhudia uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages