Mashabiki wa Yanga wakosa Uzalendo,Kilimanjaro Stars yalala 2-1 kwa Zimbabwe; - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mashabiki wa Yanga wakosa Uzalendo,Kilimanjaro Stars yalala 2-1 kwa Zimbabwe;

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti akizungumza na kituo cha Televisheni cha ITV leo, kuhusu mwenendo wa mashindano hayo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuangalia michuano hiyo.
Wachezaji wa timu za Kilimanjaro Stars na Zimbabwe wakipambana mbele ya lango la timu ya Zimbabwe wakati wa mchezo wao wa kuwania kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011.
Kikosi cha Timu ya Kilimanjaro Stars kikiwa katika picha ya pamoja.

Mashabiki wa timu ya Yanga wakifanya kitendo ambacho si cha kizalendo kwa kuishangilia timu ya taifa ya Zimbabwe wakati wa mchezo wa kuwania kuingia robo fainali ya michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii na Kilimanjaro Stars kufungwa goli 2-1 . Kitendo hicho kimelaaniwa na hata waandishi wa vyombo mbalimbali vya nje waliokuwa wakiripoti mchezo huo na kusema, "Hii haisaidii maendeleo ya soka na haijawahi kutokea katika nchi zao mashabiki wa nyumbani wakawashangilia wageni".
Mchezaji Thomas Ulimwengu wa Kilimanjaro akijaribu kumtoka Eric Mudzingwa wa timu ya Zimbwabwe katika mchezo wa kuwania kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa. Ndani ya dakika 11 timu ya Kilimanjaro Stars imefungwa goli 2 za harakaharaka na timu ya Malawi huku ikishambuliwa kwa muda mdrefu na wamalawi hao hata hivyo katika kipindi cha pili mwishoni timu ya Kilimanjaro Stars imezinduka na kufanikiwa kupata goli 1 katika dakika ya 87 kipindi cha pili. na kufanya matokeo kuwa 2-1 Hivyo kwa matokeo hayo ya 2-1 timu ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robi fainali ambapo itashuka dimbani tarehe 6 mwezi huu kucheza na timu ya taifa ya Malawi. 
Lakini jambo la kushangaza ni kwa upande mashabiki wa Yanga waliokaa upande wa kulia ambao wameonekana kushagilia vilivyo timu ya Zimbabwe, kiasi kwamba waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya nje wanashangaa inakuwaje mashabiki watanzania wako hivyo. Akifadhaika zaidi mpiga picha wa Kenya Mohamed Amin, ametoa mfano kwamba wao kwao timu yao ya taifa wanaijali na kuipenda vilivyo, tofauti na vituko vya mashabiki wa Yanga alivyoviona leo. 
Anaongeza kwa kutoa mfano kuwa "Mwaka 1987 timu yao ya Harambee Stars iliwahi kuwa na wachezaji 12 wa timu ya Golmahia, na kati ya hao 12 wachezaji 9 walikuwa wakianza kipindi cha kwanza, lakini mashabiki hawakuwahi hata siku moja kufanya kitendo cha aibu kama hiki cha mashabiki wa Yanga" amemaliza Mohamed Amin, Mwana wa mpiga picha Maarufu wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati mzee Mohamed Amin aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege miaka kadhaa iliyopita.Habari Kwa Hisani Ya Father Kidevu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages