MKUTANO WA WAWEZEKAZAJI WAWASHA KIBIRITI LONDON - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUTANO WA WAWEZEKAZAJI WAWASHA KIBIRITI LONDON


 Mh William Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini akihutubia
                     Waziri Ngeleja akiwa na Mh Naibu Balozi Chabaka wakiongea na mwananchi
 David Tarimo Tanzanian tax expert with fellow delagates-

Waziri akiwa na maafisa ubalozi na wajumbe wa jumuiya ya Watanzania London.Picha na Baraka Baraka
---
 
Wawekezaji, wataalam na wafanyabiashara toka kona mbalimbali  ulimwenguni wamekaribishwa kwa mkono wa kheri kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi yetu katika kipindi kinachofuatilia miaka 50 ya Uhuru.

Akiongea wakati wa Kongamano la Uwekezaji (Tanzania Investment Forum 2011)  hoteli bab kubwa ya  May Fair jijini London jana Ijumaa, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngeleja alisema tuko katika kipindi kipya cha maendeleo ya uchumi chenye manufaa kwa wafanyabiashara.

Waziri huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria  aliuambia mkutano kwa Kiingereza fasaha: “Miaka mitatu iliyopita Bongo imebadilika toka mnunuzi wa bidhaa kuwa muuzaji wake. Mathalan siku hizi tunaiuzia Kenya chakula. Ukilinganisha nchi yetu na nyinginezo Afrika , tumekuwa makini shauri ya amani na utulivu miaka 50 iliyopita.”

Hotuba yake mheshimiwa ilikuwa miongoni mwa hoja nyingi zilizochambuliwa na washiriki wazawa wa Uingereza, Norway, Afrika Kusini, Kenya, Marekani, Uholanzi na Tanzania.
Soma habari zaidi :

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages