Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na
mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu
alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es
Salaam leo, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua
kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi
waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo.
Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hadi sasa tayari jumla ya Maiti 38 zimekwisha opolewa majini na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na 19, kati yake mpaka sasa bado haziweza kutambuliwa.
Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hadi sasa tayari jumla ya Maiti 38 zimekwisha opolewa majini na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na 19, kati yake mpaka sasa bado haziweza kutambuliwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu
ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole
wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini
kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya
kambi za waathirika leo.
Baadhi ya wananchi walio katika Kambi hiyo, wakifua nguo zao kambini hapo.
Mmoja
kati ya watoto waishio katika Kambi hiyo ya Klabu ya Yanga, akiwa
ameuchapa usingizi katika eneo ambalo linatumika kufulia nguo, wakati
mama yake akifua nguo zake mahala hapo.
Picha ya juu inaoonyesha sehemu iliyoathirika na mafuriko hayo.
Makamu
wa Rais Dkt. Bilal, akitelemka katika Helkopta, baada ya kuzunguka
hewani na kujionea athari zilizotokea katika maeneo yaliyokumbwa na
mafuriko hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)