Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya Chakabidhi Mifuko ya Saruji 200 Kwa Ajli ya Ujenzi wa Madarasa ya shule Mbalimbali Mkoani Mbeya - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya Chakabidhi Mifuko ya Saruji 200 Kwa Ajli ya Ujenzi wa Madarasa ya shule Mbalimbali Mkoani Mbeya

M kuuwa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto),akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya  Calvin Martin mara baada ya kuwasili juzi viwanja vya Uwanja Mpya wa Ndege Songwe kwa ajili ya kukabidhiwa saruji na upandaji miti kazi iliyoratibiwa na TBL. TBL ilitoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akisalimiana na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi mara baada ya kuwasili kukabidhiwa saruji hiyo.
Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya Calvin Martin (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro sehemu ya mifuko ya saruji kati ya 200 yenye thamani ya sh.milioni 3,iliyotolewa na kiwanda hicho juzi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali mkoani humo.Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi na Meneja Mauzo na Usambazi wa TBL Kanda ya Kusini, James Kavuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto) akitoa shukurani kwa uongozi wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) baada ya kupokea msaada huo.Kulia ni Meneja UHusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi na Meneja Mauzo na Usambaji wa TBL Kanda ya Kusini James Mavuna na Meneja wa Kiwanda cha Bia Mkoa wa Mbeya Calvin Martin.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages