

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa
Mtangazaji wa TBC, David Wakati, alipofika nyumbani kwa marehemu huyo Oysterbay
jijini Dar es Salaam jana Desemba 2, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole.
Marehemu Wakati alifariki juzi jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na ndugu wa marehemu David Wakati, Francis Wakati, ,
Josephine Wakati (katikati) na Elizabeth Wakati, baada ya kumaliza kutia
saini katika kitabu cha maombolezo, alipofika kutoa mkono wa pole kwa
nyumbani kwa familia ya marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam jana
Desemba 2.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)