Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
wananchi walioathirika na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar hapo
katika ukumbi wa Chuo cha Karume Mbweni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na
kushoto yake ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundo Mbinu Mh. Issa
Haji Ussi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifafanua lengo la
Serikali la upanuzi wa uwanja wa kisasa wa ndege kwa nia ya kuongeza
mapato ya taifa
Wananchi
walioathirika na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar wakimsikiliza
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo ukumbi wa
chuo cha Karume Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
---
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imeombwa kuhakikisha kwamba utaratibu muafaka
usioleta machungu unazingatiwa ili kuwapa faraja Wananchi walioathirika
na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Kauli
hiyo imetolewa na Wananchi hao katika mkutano maalum wa kujadili
mvutano uliojitokeza kati ya Wananchi hao na Uongozi wa Mamlaka ya ndege
kuhusu upanuzi wa uwanja wa ndege ambao unalazimika nyumba na vipando
vilivyomo katika eneo hilo viondolewe.
Mkutano
huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Karume Mbweni ulisimamiwa na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.Wananchi hao
walisema mizozo mingi inaibuka kutokana na baadhi ya watendaji wa
Serikali kutokuwa waadilifu kitendo ambacho kinawaondoshea imani.
Walisema
tabia za baadhi ya watendaji kuchelewesha utaratibu wa ulipaji wa fidia
katika awamu za mwanzo za upanuzi wa Uwanja huo zitasababisha ufukara
unaoweza kuepukika.
“
Hii ni Serikali yetu wenyewe kwa sababu walioko madarakani ni miongoni
mwetu sisi. Hivyo ni vyema lile tunaloliomba kwa maslahi yetu na vizazi
vyetu likazingatiwa ili kukinga mzozo ”. Alisema mmoja wa Wananchi hao
Nd. Ramadhan Mrisho Rupia.
Wananchi hao walitahadharisha zaidi kuzingatiwa kwa hatma yao ya baadae ambayo ni muhimu katika maisha yao.
Akizungumza
na Wananchi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali kamwe haikusudii kuwafanyia ubabe wananchi wake.Balozi
Seif alisema maamuzi ya Serikali wakati wote yanalenga katika kuona
maendeleo yanaifikia Jamii yote ingawa baadhi yao wnaweza kuathirika na
Hatua hizo.
“ Kama tunahitaji Maendeleo ni lazima inabidi tutumie rasilmali zetu wenyewe ”. Alisema Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wananchi hao kwamba
malalamiko yao atayawasilisha katika ngazi za juu kwa lengo la
kuzingatiwa zaidi.Balozi Seif ameahidi kufuatilia malipo yote ya fidia
ya Wananchi ambao hawajapatiwa katika upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa
awamu zilizopita.Hata hivyo makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alisisitiza kwamba Ardhi itaendelea kuwa mali ya Serikali kutokana na
Historia ya Nchi hii ilivyokuwa.
Upanuzi huo wa Uwanja wa ndege wa Zanzibar una ukubwa wa Square Metre laki 928,268.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)