Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Handeni
.
Mahakama ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewahukumu Raia 103 wa
Somalia, kwenda Jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kuingia nchini
kinyume cha sheria.
Mbele
ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Handeni Jonathan Mgongolwa, mwendesha
mashitaka wa Idara ya uhamiaji wilayani humo ASP Charles Kasambula,
alidai kuwa wasomali hao walikamatwa na Polisi katika maeneo mawili
tofati wilayani humo wakiwa njiani kuelekea nchini Malawi bila ya kufuta
taratibu za kiuhamiaji.
Watuhumiwa
wote walikiri shitaka hilo na Hakimu Mgongolwa akaamru kuwahukumu
kwenda Jela mwaka mmoja na kwamba mara wamalizapo kifungo chao,
wasomali hao wasafirishwe kurudishwa makwao katika nchi waliotoka.
Wakati
wa hukumu hiyo, Hakim Mgongolwa amesema amelazimika kutoa adhab hiyo
ili iwe fundisho kwa wageni wengine wanaotaka kuingia hapa nchini
kufuata taratibu na sheria zikiwemo zile za kimataifa zinazomlazimu kila
mgeni kuheshimimu mipaka na taratib za nchi anayopanga kuingie ama
kupitia akiwa njiani kuelekea katika taifa lingine.
Wasomali
hao hao ambao wote ni waname wenye umri kati ya miaka 20 na 30,
walikamatwa na Polisi wilayani Handeni mwishoni mwa wiki iliopita wakati
wa operesheni maalum ijulikanayo kama funga mwaka bila uhalifu inayoendeshwa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Katika
hata nyingine Jeshi la Polisi mkaoni Tanga limesema linafuatilia
nyendo za mawakala wanaopokea wahamiaji haram na kwasafirishwa kwa
magendo kwenda katika mataifa mengine.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo ACP Costantino Masawe, amesema kuwa pamoja na
mawakala hao, pia Polisi inayafuatilia magri ya mizigo na madereva
wanaotumika kuwasafirisha wasomali hao ili wakamata na kuwafikisha
mahakamani.
Kamanda
Masawe amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi ili
kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu vikiwemo vile vya
usafirishaji haramu wa binadam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)