Vifaa
vya Kivita vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikiwa katika
mazoezi ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru
kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. Sherehe hizo zinafikia
Kilele cheke kesho ambapo shughuli zote zitafanyika katika Uwanja huo
wa Uhuru ambapo sherehe za mkesha wa sherehe hizo zitaanza leo katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja Mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Magari ya Kivita na Vifaa vya kivita yakipita mbele ya jukwaa Kuu wakati wa mazoezi ya Wanajwtz.
Kila aina ya gari la Kivita lilipita wakati wa mazoezi hayo.
Vijana wa Scout wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya sherehe hiyo kwenye Uwanja huo huo wa Uhuru.
Mazoezi yanaendelea uwanjani hapo.
Ni mazoezi ya vijana hao Chipukizi wakijifua na mazoezi ya silaha.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)