 |
|
MWENYEKITI
wa Shirika la Ushirikiano wa Tanzania na nchi ya China SINOTA
Friendship Association Bw. Jiang Jing Ying leo asubuhi alishindwa
kuvumilia na kujikuta akimwaga machozi baada ya kukutana na wastaafu
wenzie waliofanyakazi pamoja Reli ya TAZARA miaka zaidi ya 40 iliyopita
|
 |
|
Bw.
Jing alikutana na wastaafu hao wa TAZARA na kuona hali zao za maisha
ambapo mara baada ya kumaliza kusalimiana nao alianza kumwaga machozi
akikumbuka namna ambavyo aliishi nao miaka hiyo huku wakiwa katika hali
mbaya ya maisha tofauti na jinsi yalivyo maisha yake nchini China.
|
 |
|
Alisema
kuwa ushirikiano uliodumishwa na marais wastaafu wa Tanzania Hayati
Mwalimu Nyerere wa Tanzania na Hayati Mao Tse Tung wa China unapaswa
kuendelezwa kwa kudumisha rasilimali zilizoachwa ikiwemo reli ya TAZARA
ambayo inapaswa kutunzwa.
|
 |
|
Bw.
Ying ambaye pia ni Mkurugenzi wa makampuni kadhaa nchini China anasema
kuwa hakutegemea kuwaona watu aliofanya nao kazi wakiwa katika hali duni
ya maisha huku wengine wakiwa wamezeeka wakionekana wakishindwa
kuendesha maisha yao kutokana na hali ngumu ya uchumi waliyonayo.
|
 |
|
Alisema
kuwa reli ya TAZARA imechakaa hali ambayo inaweza kusababisha kuibuka
kwa ajali jambo ambalo linaweza kugharimu maisha ya watu, hivyo
alishauri kuwepo na mikakati mbadala ya kuirejesha reli ya TAZARA katika
hadhi yake kama ilivyokuwa miaka ya sabini.
|
Bw.
Ying anakumbuka alivyofanya kazi kuanzia Kurasini Jijini Dar es salaam
kati ya mwaka 1969 na baadaye Kisarawe kisha alihamia Mbeya na Mbozi
hadi Tunduma ambako,amepanga kufanya ziara ya kuitembelea reli hiyo
kuanzia Tunduma hadi Dar es salaam ambako amepanga kukutana na Rais
Jakaya Kikwete ili amweleze mambo muhimu juu ya uboreshaji wa reli
TAZARA.Habari Kwa Hisani Ya Mbeya Yetu Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)