HAFLA YA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU USIKU HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HAFLA YA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA YAFANA VIWANJA VYA IKULU USIKU HUU

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha UDP Bw. John Momose Cheyo katika hafla ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania iliyofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, huku mtandao wako wa FULLSHNAGWE ukikuletea matukio haya kutoka viwanja vya Ikulu moja kwa moja.
Wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, Mawaziri, Wabunge na Mabalozi na waalikwa mbalimbali wamehudhuria katika hafla hiyo iliyokua na burudani za vikundi vya ngoma kutoka sehemu mbalimbali.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati alipokuwa akipita sehemu mbalimbali na kuwasalimia katika viwanja vya Ikulu huku akiwatakia sherehe njema ya miaka 50 ya Uhuru.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka Viwanjani Bw. Alex Msama ambaye naye alihudhuria katika hafla hiyo.
Waimbaji wa muziki wa injili nao wamehudhuria katika hafla hiyo kama wanavyoonekana katika picha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages