Washiriki
wa shindano la Mitumbwi 'Balimi Extra Lager' wakiwa majini wakichapa
mwendo wakati wa shindano hilo lililofanyika eneo la Mwaloni jijini
Mwanza jana.
Sehemu ya wakazi wa Jijini Mwanza wakishuhudia mashindano ya Mitumbi ya Balimi Extra Lager Mwaloni Jijini Mwanza jana.
Wakazi wa Jijini Mwanza wakishuhudia mashindano hayo.
Washindi
wa kwanza upande wa wanawake,Kikundi cha Teddy Totto kutoka Nansio
Ukerewe wakiwasili Mwaloni wakati wa mashindano ya Mitumbwi Balimi Extra
Lager yaliyomalizika.
Washindi
wa kwanza upande wa wanaume,Kikundi cha Martin Mwarabu kutoka Nansio
Ukerewe wakiwasili Mwaloni wakati wa mashindano ya Mitumbwi Balimi Extra
Lager yaliyomalizika jana.
Washindi
wa kwanza upande wa wanawake wakikabidhiwa zawadi yao ya kitita cha
Shilingi Milioni 2,200,000 ambao ni kikundi cha Teddy Titto kutoka
Nansio Ukerewe.
Na Michael Machellah, Mwanza
NANSIO Ukerewe waibuka mabingwa na
kujinyakulia jumla ya Sh. Miliioni 4,800,000, katika Fainali za
mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager yaliyomalizika jana eneo la
Mwaloni Jijini Mwanza.
Fainali
za mashindano haya yalikuwa ya Kanda ya ziwa ikishilikisha jinsia zote
ya keke na kiume,ambapo Ukerewe waliibuka washindi kwa jinsia zote kwa
wanaume kikundi cha Martin Mwarabu kutoka Nansio Ukerewe na kujipatia
zawadi ya Shilingi Milioni 2,600,000, na kwa upande wa wanawake Kikundi
cha Teddy Totto cha Nansio Ukerewe pia kiliibuka na ushindi na
kuzawadiwa Shilindi milioni 2,200,000.
Matokeo
hayo kiliyafanya mashndano kuwa na shamrashamra za kushangilia kwa aina
yake kwa ngoma ndelemo na vigelegele toka kwa wakazi wa Ukerewe
walitoka Ukerewe na Wakewe waishio Mwanza hivyo kukifanya Kitonjoji cha
Mwaloni kujaa ndelemo na vifijo.
Mshindi
wa pili kwa wanaume walikuwa ni kikundi cha Umoja kutoka Bukoba ambao
walizawadiwa Shilingi 2,000,000, wa tatu ni kikundi cha Kisolya kutoka
Msoma ambao walizawadiwa Shilingi milioni 1,600,000 na wa nne ni
kikundi cha Nyalusulya kutoka Musoma na washiliki wa tano hadi wa kumi
walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 400,000 kila kikundi, ambavyo ni
Kanchakwizi kutoka Bukoba,Elisha Jacob cha Mwanza,Godfrey Ignatus
chaNansio Ukerewe,Rwekaza kutoka Bukoba,Matinika Hangaika kutoka Mwanza
na cha Shija Andrew kutoka Mwanza.
Mshindi
wa pili kwa wanawake walikuwa ni kikundi cha Kinesi kutoka Musoma
ambacho kilipata Shilingi 1,600,000,cha tatu ni kikundi Mfunda Mfunda
Mbogo kutoka Mwanza na cha nne ni cha Happiness Mnare kutoka Mwanza na
vikundi vingine cha tano hadi kumi walizawadiwa kifuta jasho Shilingi
200,000, kila kikundi ambavyo ni Rwagasire kutoka Musoma,Tindichebwa
Mganga kutoka Mwanza,Busira kutoka Bukoba,Seleka kutoka Bukona,Paskazia
Shukurani kutokaNansio Ukerewe na cha Elizabeth Charles kutoka Mwanza.
Mashindano
hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Evarist Ndikilo ambaye
ndiye akikuwa mgeni rasmi akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya, Said Amanzi
na kiongozi mwenyeji kutoka Kampuni ya Bia Tanzania walikuwa ni Meneja wa
Bia ya Balimi iliyodhamini mashindano, Edith Bebwa na Meneja mauzo na
usambazaji wa Kanda, Malaki Staki.












No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)