Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Phillip Marmo,
kuwa Balozi wa China, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya
iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Marmo awali alikuwa ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
Mabalozi wapya waliofia Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, wakisubiri kuapishwa.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Batilda Buriani, kuwa
Balozi wa Kenya, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya
iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Batilda awali alikuwa ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Rais
Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Deodorus Kamala, kuwa Balozi wa
Ubelgiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya
iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Kamala, awali alikuwa ni
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rais
Jakaya Kikwete, akimwapisha, Ally A. Saleh, kuwa Balozi wa Oman, wakati
wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika mchana huu,
Ikulu Dar es Salaam. Saleh, awali alikuwa ni Balozi Mdogo wa Dubai.
Rais
Jakaya Kikwete, akimwapisha, Shamim Nyanduga, kuwa Balozi wa Msumbiji,
wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo
mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Nyanduga awali alikuwa ni Naibu Mkuu wa
Itifaki, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Samim
Nyanduga, akipongezwa na Mumewe, baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi
wa Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
Nyuma yao ni wanafamilia wa Familia hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda (kuli) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe, wakizungumza jambo, baada ya kumalizika kwa
hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam
leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Benard Membe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika picha ya pamoja na
Mabalozi wapya baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam.














No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)