Bw.
Martin Masaly Afisa Mtafiti wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
akitoa maelezo kuhusu kazi na masuala ya uwekezaji Tanzania kwa Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa alipotembelea banda hilo. Kulia ni
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa (Katikati) akipokea maelezo ya
Uwekezaji na Uwezeshaji kutoka kwa Bw. Suleiman Malela Mkaguzi wa Ndani
wa Baraza la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi, alipotembelea banda hilo.
Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa Afisa
Mtafiti Bw. Martin Masalu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, tarehe 3/12/2011 Jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa maelezo kuhusu
masuala ya Maafa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa
alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika maadhimisho ya
Kitaifa ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K
Nyerere vilivyopo Kilwa Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. John Malecela akinunua Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika
maadhimisho ya Kitaifa ya MIaka 50 ya Uhuru yanayofanyika katika Viwanja
vya Mwl. J.K Nyerere vilivyopo Kilwa Dar es Salaam. Kushoto ni
Mpigachapa Bibi. Joyce Benjamin wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa
Serikali.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akipata maelezo kuhusu Idara na
Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu zilizoshiriki katika maonesho ya Miaka
50 ya Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. David Kirway alipotembelea Banda hilo katika
Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere tarehe 3/12/2011 Jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)