Mwenyekiti Wa Chama Cha Demokkrasia Na Maendeleo Freeman Mbowe
Na Mwandishi Wetu, Mvomero
DIWANI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Mtibwa,
Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi.Tusekile Mwakyoma (28), amechomwa kisu chini ya ziwa la kushoto na mchumba wake Mkurugenzi wa Mafunzo na
Uenezi wa chama hicho, Bw.Songa Mgweno, mkazi wa Kijiji cha Kilimanjaro,
ambaye alitoweka baada ya tukio hilo.
Akizungumza na Majira akiwa wodini katika Hospitali ya Misheni
Bwagala, Bi.Mwakyoma alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana
ambapo Bw.Mgweno, alikimbia na fedha zake sh.200,000.
“Huyu Bw.Mgweno ambaye ni mchumba wangu, alinipigia simu saa mbili usiku niende nyumbani kwake Kijiji cha Kilimanjaro ili nikachukue fedha zangu, niliamua kulala huko na ilipofika alfajiri, aliniamsha na kuniuliza nimefanya juhudi gani kuhakikisha wazazi wangu wanakubali anioe lakini nilimwambia sina jibu.
“Huyu Bw.Mgweno ambaye ni mchumba wangu, alinipigia simu saa mbili usiku niende nyumbani kwake Kijiji cha Kilimanjaro ili nikachukue fedha zangu, niliamua kulala huko na ilipofika alfajiri, aliniamsha na kuniuliza nimefanya juhudi gani kuhakikisha wazazi wangu wanakubali anioe lakini nilimwambia sina jibu.
“Tuliendelea kulala lakini baada ya muda, alianza kunipapasa
nikasikia maumivu makali chini ya ziwa la kushoto, baada ya
kujichunguza, nikaona kisu kikining'inia,” alisema.
Aliongeza
kuwa, Bw.Mgweno alimkaba koo na kuchomoa kisu hicho ili ampige kingine
lakini alijitahidi kumdhibiti huku akipiga kelele kuomba msaada ambapo
ndugu wa mwanaume waliamka na kwenda chumbani kwao kutoa msaada.
“Walipofika chumbani, walikuta Bw. Mgweno tayari amekimbia kupitia mlango wa nyuma,” alisema Bi. Mwakyoma.
Kwa
upande wake, mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani hapa, Bw.Hamisi
Selemani, alisema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili
aweze kufikishwa mahakamani.
Mama wa Bi.Mwakyoma ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara
moja, alisema walimkataza mtoto wao asiendeleze uhusiano na Bw.Mgweno
kwa sababu alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine ambaye ni kabila
lake.
Baadhi ya wapiga kura katika kata hiyo, wamewaomba viongozi wa CHADEMA
Taifa kumfukuza uanachama Bw.Mgweno kutokana na kosa alilofanya la
kumshambulia diwani wao na kutaka kumuua.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)