katibu kata wa kijiji cha Mtii bwana Reginald Mlay Akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mnara wamasiliano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ulioko katika kijiji cha Mtii wilayani same Mkoani Kilimanjaro, akishuhudia kushoto ni Afisa mtendaji wa kata bwana Filbert Salim Mgamba.
Alhamisi 15 Decemba 2011, kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel wiki hii imezindua huduma za mawasiliano katika kijiji cha Mtii wilayani Same mkoani Kilimanjaro na kuwafikishia wakazi wa vijiji vya jirani vya Mtae, Kanza, Bombo na Vunda huduma ya mawasiliano.
Huduma za mawasiliano zilizinduliwa rasmi na katibu Tarafa wa Mtii Bw. Reginald Mlay na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo, wafanyakazi wa Airtel , waandishi wa habari na wakazi wa kijijini hapo ambapo bwana Reginald alisema " tunachukua fulsa hii kuwapongeza na
kuwashukuru Airtel kwa kufikisha mawasiliano kijijini hapa, huduma hizi zitachangia kwa kasi maendeleo ya wananchi na kurahisisha mawasiliano kuwa rahisi, sasa wakazi wa Mtii na vijiji vya Mtae, Kanza, Bombo na Vunda wataweza kupata mawasilioano mazuri ili kufanya kibiashara na kuwezesha bidhaa zao kupata masoko kirahisi, hivyo basi tunawaasa wakazi wa vijiji hivi kutumia nafasi hii katika kuboresha shughuli zenu za kilimo na biashara".
Tunauhakika pia ulinzi wa wananchi na mali zao utaimarika zaidi kwa mawasiliano haya rahisi na yenye uhakika kupitia mtandao wa Airtel.aliongeza Mlay. Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja Mauzo msaidizi wa kanda ya Kaskazini bw. Pascal Bikomagu alisema "Airtel imewekeza kiasi kikubwa katika kujenga minara ya mawasiliano na kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wakazi wote nchini hasa walioko vijijini ambapo mawasilino yasimu ni changamoto kubwa. Kwa mwaka huu mpaka sasa zaidi ya maeneo tofauti yanayofikia 167 mapya yameweza kufikishiwa huduma nchi nzima.
Dhamira yetu ni kuwafikia wananchi wote katika maeneo mbalimbali ya nchi hii. Tumetimiza na kuthibitisha dhamira yetu leo hii kwa kuzindua huduma zetu hapa kijijini cha Mtii na kuwawezesha wakazi wa kijiji cha hapa na vijiji vya jirani wapatao 25,000 kuweza kupata huduma zetu".
Sasa wakazi na wateja wetu wa Mtii wanaweza kupata huduma zetu zinazopatikana nchi zima kwa kuhamia Airtel sasa huduma hizi ni kama vile za pesa mkononi kutuma na kupokea fedha kupitia"Airtel Money" , huduma za internet, na kupiga simu kwa viwango nafuu zaidi nchi nzima. Akiongea baada ya uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema " Ni wiki mbili tu zimepita tangu Airtel Tufikishe wateja wetu wa milioni 50 kwa Afrika, hii inaonyesha dhahiri kuwa bidhaa na huduma tunazotoa ni muhimu na zinasaidia jamii zote tunazozihudumia na ndio maana wateja wanaichagua Airtel. Mkakati tulionao ni kuendelea kuongeza huduma bora ili kuendelea kuwapatia wateja wetu huduma bora pamoja na kuongeza ubunifu kwenye ujio wa bidhaa mpya ili kuwafaidisha wateja na kampuni kwa ujumla Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboresha maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina na huduma mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo. Airtel inachangia shughuli za afya, elimu na mazingira ili kuhakikisha jamii inayoipatia faida inazidi kuendelea na koboresha maisha yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)