WAZIRI EZEKIEL MAIGE AKIWA KWENYE ZIARA MOSHI NA KILIMANJARO! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI EZEKIEL MAIGE AKIWA KWENYE ZIARA MOSHI NA KILIMANJARO!

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (watatu kulia) akielekezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Feetham F. Banyikwa jinsi ya kulenga shabaha na moja ya bunduki zinazotumika na askari wanyamapori kukabiliana na wanyama waharibifu na doria, Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho. Picha na Tulizo Kilaga
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (aliyeshika bunduki), akipewa maelezo juu ya aina za bunduki zinazoruhusiwa kutumika katika shughuli za uwindaji wanyamapori na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka, Prof. Feetham F. Banyikwa, Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho. Picha na Tulizo Kilaga
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (kulia) akipanda mti katika viwanya vya Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita na kushoto ni mwanafunzi wa chuo hicho Grace Lyimo. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (kulia) akipanda mti katika viwanya vya Chuo cha Uhifadhi Wanyamapori Mweka, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita na kushoto ni mwanafunzi wa chuo hicho Grace Lyimo. Mhe. Maige alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 46 ya chuo hicho. 
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Ibrahim Mussa (kulia) akimsisitizia jambo mwekezaji wa sekta ya utalii, Robert (kushoto) katika Ziwa Chale, Rombo, Kilimanjaro alipofanya ziara wilayani humo kuangalia maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Hoteli za Kitalii huku Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (katikati) akisikiliza kwa makini, Rombo, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages