- LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya


 Wanamuziki wa Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Alfajiri wakati wakiondoka nchini kuelekea Uingereza ambao wanakwenda kufanya maonyesho kadhaa, ambapo onyesho lao la kwanza linatarajia kuanza kesho jijini humo.
********************************
Twanga Pepeta ''KISIMA CHA BURUDANI'' wameondoka leo asubuhi kutoka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere wakienda kuwasugulisha Kisigino wapenzi wao walioko katika Jiji la London nchini Uingereza na nchi jirani ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
 Kundi hilo lililokamilika katika safu zake za waimbaji, wapiga vyombo na wacheza show linatarajiwa kuwasha moto wa burudani yao siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Club 2000 Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB kuanzia saa Tatu Kamili Usiku mpaka alfajiri (9pm til late).
Mheshimiwa Balozi Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. CD za album mpya na za zamani zitauzwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kitanzania vitakuwepo vya kumwaga. Viingilio vitakuwa £20 (singles) na £35 (couples) kabla ya saa sita (mid night) na £25 (singles) na £40 (couples) baada ya saa sita usiku.
Njoo tujumuike, njoo usugue kisigino, njoo usherehekee uhuru wa nchi yako, njoo ule na kunywa kitanzania. Burudani ni watu na watu ni pamoja na wewe. Tanzania itajengwa na watu wenye moyo kama wewe. Karibuni sana.
 Kiongozi wa bendi hiyo, Charls Baba (katikati) akipozi na mpiga solo wake, Shakashia pamoja na Mnenguaji, Shalapova.
Mpiga Kinanda wa Bendi hiyo, Victor Mkambi akipozi na Mnenguaji, Maria Soloma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages