Utambulisho wa Uhuru's Wings: Freedom to Fly yaani, Mbawa za Uhuru: Uhuru wa upaa! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Utambulisho wa Uhuru's Wings: Freedom to Fly yaani, Mbawa za Uhuru: Uhuru wa upaa!


Uzuri na ustadi wa utamaduni wa Kimasai ni maarufu na hupendwa na wengi duniani na si Afrika Mashariki pekee. Hivi karibuni tumeshuhudia wanamitindo wengi hapa nchini na katika majukwaa ya kimataifa wakiutumia kama chanzo na zinduko la maonesho yao. Shanga za kimasai zimepamba na kupendezesha mengi kwa miaka mingi kabla ya wanamitindo na wanasanaa duniani kuvutiwa nazo. Kanga, Vitenge na mashuka ya wamasai zimekuwa ni mojawapo ya mitindo ya kitanzania kabla ya mitindo ya kiafrika kuwa mitindo ya hali ya juu yaani ‘couture’. Lakini, hivi karibuni tumeshuhudia yote haya katika majukwaa ya mitindo ya kimataifa na pia katika halaiki za mitindo.

Halaiki ya kwanza kutoka katika nyumba ya mitindo ya mapambo ya vito na vipodozi vya mwili: Heart 365 Emporium inaitwa Uhuru's Wings: Freedom to Fly. Mvutio wa kutengeneza mapambo haya umetokana na utamaduni wa Kimasai. Jambo hili limekusudiwa na mwanzishi wake, Jacqueline Kibacha aliyetaka kuonesha uzuri wa nchi yake ya asili, Tanzania na pia kushirikisha dunia katika kile ambacho ni chetu sote – utamaduni wetu. Heart 365 itawasaidia wamasai wenyewe kwa kutoa kiasi cha mauzo yake katika kituo cha Emusoi

Uhuru's Wings: Freedom to Fly ilizinduliwa mwanzo wa mwezi huu katika shughuli  ya hisani iliyoandaliwa na UK Comic Relief. Shughuli hiyo inajulikana kama: See Africa Differently. Tafadhali tembelea www.heart365.co.uk ili ujionee mitindo ya mapambo ya vito hivyo.
 
kilichopo Arusha. Kituo cha Emusoi hujenga mfuko wake kutokana na misaada ambayo hutumika kuwaendeleza wasichana wa kimasai wenye umri wa kusoma katika shuke za sekondari kwa kuwasomesha na kuwafundisha kazi.
Kwa habari zaidi waandikie: info@heart365.co.uk

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages