TAMASHA LA STREET UNIVERSITY LAWEKA REKODI ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAMASHA LA STREET UNIVERSITY LAWEKA REKODI ARUSHA


Eric Shigongo akitoa mada za ujasiriamali na namna ya kujikomboa na umaskini kupitia biashara.
Msanii wa muziuki wa injili, Pastor Wambura wa Arusha akifanya vitu vyake jukwaani.
 James Mwang’amba akitoa mada za ujasiriamali na namna ya kujikomboa na umaskini kupitia biashara.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Bonny Mwaitege na Christina Shusho wakitoa burudani jukwaani kwenye tamasha hilo.
Wasanii wa kundi la muziki wa injili la Dot Com Generation wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mtoa mada mkuu katika tamasha hilo, Eric Shigongo akibadilishana mawazo na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema wakati wa tamasha hilo.
Mratibu wa Tamasha hilo, James Mwang’amba,(katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini -Chadema Mheshmiwa Godbless Lema.
Msani wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Kinzasa ‘20%’ akifanya vitu vyake kwenye tamasha hilo.
Sehemu ya umati uliohudhuria tamasha hilo.
  --
Tamasha kubwa la ujasiriamali la Street University lililofanyika kwakishindo ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumapiliiliyopita, limeweka rekodi kwa kulifanya jiji hilo litingishike kwaburudani kabambe kutoka kwa wasanii kibao waliokamua jukwaani pamoja
na mada motomoto za ujasiriamali zilizotolewa.

Risasi mchanganyiko lilikuwepo kwenye uwanja huo na kushuhudia jinsiumati uliofurika, wakiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema naaskofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie walivyoyafurahiamafunzo ya ujasiriamali na burudani ya kukata na shoka iliyoporomoshwana wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina
Shusho, Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’ , Glorious Singers,Dot Com Generation na Pastor Wambura.

“Tumepata mwitikio mkubwa kuliko hata tuliuvyotegemea. Tunawashukurusana wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kwa kutuunga mkono nakujitokeza kwa wingi kusikiliza tulichowaandalia. Tunaamini maisha yawengi yatabadilika kwani tumepandikiza mbegu za ushindi na mafanikio maishani.

“Tunawashukuru sana wadhamini waliowezesha kufanyika kwa tamasha letu, Kampuni ya Global Publishers Ltd, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple ARadio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM),Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM)  na Radio 5 (105.7FM), zote za jijini Arusha,” alisema Mwang’amba ambaye ndiye aliyekuwa mratibu watamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages