Masoud Kipanya akiwa amepozi kwenye kaunda suti yake na si gwanda/vazi la CHADEMA.
UPUUZI
WA MASOUD KIPANYA ni documentary ya dakika 47 ambayo nimeirekodi mwaka
juzi katika mazingira ya kijiji kilichotumika kurekodia MAISHA PLUS.
Mfumo
nilioutumia ni kuongelea mambo mengi mchanganyiko na ili kuondoa uchovu
wa kunitazama nikiongea, nimechanganya footages za videos,
illustrations na animation (katuni) kuchagiza yale ninayokuwa
nayazungumzia.
Ujumbe
wa dvd hii ni nadharia ya vipande 26 vya keki. nikatengeneza MFANO wa
uwepo wa idadi hiyo ya vipande vya keki ambavyo mara baada ya kuwekwa
mbele ya watu (watanzania), kundi hilo la watu likataka kutoana roho ili
kila mmmoja apate kipande cha keki hiyo, bahati nzuri wakatokea werevu
(viongozi) ambao waling'amua kuwa kumbe idadi ya vipande vya keki (26)
ni sawa kabisa na idadi ya watu waliokuwepo ambao walikuwa wanakaribia
kutoana roho.
Werevu
hawa wakawaambia watu hawa kuwa hatuna haja ya kung'oana meno wakati
idadi yetu ni sawa kabisa na vipande vilivyopo, ukatengenezwa uataratibu
wa kupanga foleni ili kila mmoja apite mbele achukue KIPANDE chake.
baada ya kukubaliana hilo, bado werevu wakaona ni vema foleni hii
iangalie walio dhaifu ili wawe mbele wawahi kupata keki kuchelea
kuanguka kwa njaa.
Wakati
vipande hivi vya keki vilipoanza kugawiwa, hawa viongozi, (watatu)
wakaamua nao kwa kuwa ni sehem ya watu 26 kuchukua VIPANDE VYAO MAPEMA,
bahati mbaya baadhi yao kutokana na kuwa karibu na meza ya keki na
kutokana na ULAFI, wakaamua kuchukua zaidi ya kipande kimoja cha keki
hali iliyopelekea watu wa mwishoni katika foleni ile kukosa vipande
vyao.
dvd
hii pia imeingia ndani kwa mafumbo kiasi kuangalia sababu inayopelekea
watu kutaka kujipendelea zaidi kiasi cha kupelekea kudhulumu wengine,
ikajaribu pia kuangalia dawa inayoweza kutumiwa kuepuka hali hii ya uchu
na tamaa inayosababishwa na hofu ya kujiuliza nitapata lini na woga wa
kuhofia kupoteza kidogo alicho nacho mkononi.
Kwanini
umeitwa upuuzi? kwa sababu ya tabia na hulka za binaadam kupenda
kupuuza kila kitu, ni hili nalo limetengenezwa ili ulitazame kisha
ulipuuze.
Concept: Ni documentary yenye sauti na picha za video pamoja na katuni mnato na katuni mtembeo (still cartoons and animation)
Wahusika wakuu: Masoud Kipanya
Itaingia lini sokoni: imeingia sokoni jana jumanne tarehe 15-11-2011 na inasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL.
Bei: Shilingi 3,000 tu.
Running time: Dakika 47
Sponsors: Hakuna mdhamini.
Future plans: Ni matayarisho ya upuuzi mwingine "WENYE NGUVU NA WAPAGAZI"
Nashukuru kwa ushirikiano wenu na mungu awabariki sana
MASOUD KIPANYA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)