Taswira Mbalimbali Za Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Mashariki Ya Kati - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Mbalimbali Za Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Mashariki Ya Kati

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi,mwenyeji wake Kiongozi wa Ras Al Khaimah,wakati alipowasili katika kasri ya kiongozi huyo Mjini Ras Al Kahimah, jana akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano wa mashirikiano na kukuza maendeleo ya sekta mbali mbali za maendeleleo,kama Afya,Elimu,Biashara nyenginezo za maendeleo.(12/11/2011)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(wapili kushoto)akiwa pamoja na Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi,wakishuhudia utiaji saini makubaliano kuhusu ushirikiano wa kukuza sekta mbali mbali za maendeleo,ambapo kwa upande wa Zanzibar Waziri wa kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Mhe Haroun Ali Suleiman,na Sheikh Abdullah Bin Humaid Al Qasimi kwa upande wa Ras Al Khaimah,saini hizo zimetiwa katika ukumbi wa kasri ya Sheikh Soud.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi,mwenyeji wake Kiongozi wa Ras Al Khaimah,wakati alipowasili katika kasri ya kiongozi huyo Mjini Ras Al Kahimah jana akiwa katika ziara ya kukuza uhusiano wa mashirikiano na kukuza maendeleo ya sekta mbali mbali za maendeleleo,kama Afya,Elimu,Biashara nyenginezo za maendeleo. 
Kwa Picha Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages