Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mjumbe wa
Kamati Kuu
na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha China Liu
Yunshan (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Chama
hicho na Ujumbe wa CCM baada ya kuwa na mazungumzo, Ikulu mjini Dar es
Salaam, jana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mjumbe wa
Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha
China Liu Yunshan baada ya mazungunzo yao Ikulu mjini Dar es Salaam,
jana. Walioko nyuma, kutoka kiushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Pius Msekwa (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama (kulia)
na wengine ni Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Martine
shigella, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC,
Mambo ya Nje Januari Makamba na Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha
Abdallah Juma.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha
Kikomunisti cha China, Liu Yunshan (wapili kulia) akipatiwa maelezo na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kichina ya StarTimes William Lan
alipotembelea kampuni hiyo, Mwenge, Dar es Salaam. Kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Watatu kushoto ni Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye ambao walifuatana na kiongozi huyo.
Nape akiungana na wasanii wa kundi la Tanzania House Of Talent
(THT) kucheza ngoma, kundi hilo lilipokuwa likiyumbuiza katika ziara ya
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha
Kikomunisti cha China Liu Yunshan (hayupo pichani) kwenye ofisi za
kampuni ya StarTimes, Mwenge Dar es Salaam, jana
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye akimtuza fedha msanii Hassan Kasim wa kikundi cha Tanzania
House Of Talent baada ya kuvutiwa na uhodari wa kucheza sarakasi wa
msanii huyo, kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika ziara ya Mjumbe
wa Kamati Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi Chama Cha Kikomunisti cha
China Liu Yunshan (hayupo pichani) kwenye ofisi za kampuni ya
StarTimes, Mwenge Dar es Salaam, jana.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye akitazama wanyama mbalimbali waliokaushwa kitaalam waliopo katika
Nyumba ya Sanaa, alipofika katika kituo hicho akiwa na Mjumbe wa
Kamati Kuu na Mkuu wa Iadara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha
China Liu Yunshan, jana.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Sanaa Dar es Salaam, Dk.
Paul Msemwa (kulia) akimpa maelezo kuhusu viumbe hai, Mjumbe wa Kamati
Kuu na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama Cha Kikomunisti cha China, Liu
Yunshan (wapili kushoto) aliyetembelea Taasisi hiyo ya jana. Kushoto
ni Mwenyeji wa mgeni huyo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape
Nnauye.
Picha zote na Bashir Nkoromo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)