TAMASHA LA INJILI LA SIFA ZIVUME KUFANYIKA NOVEMBA 27/2011 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TAMASHA LA INJILI LA SIFA ZIVUME KUFANYIKA NOVEMBA 27/2011

Mratibu wa tamasha la SIFA ZIVUME,pichani kulia,Mchungaji Safari akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kuhusiana na tamasha hilo,linalotarajiwa kufanyika jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. DarMchungaji Safari amesema kuwa katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni 5000 kwa viti vya kawaida na shilingi 10,000 kwa viti maalum,aidha ameongeza kuwa tiketi hizo zinapatikana DPC Kinondoni,Mlimani City,Silva Spoon,Mwenge Christian Bookshop,CLC Bookshop mtaa wa Mkwepu,Mbogo Shop Kariakoo na Mars Collection karibu na Posta ya zamani. Mchungaji Safari alibainisha kuwa mbali ya kundi hilo pia kutakuwepo na makunndi mengine yatakayotumbuiza kama vile The Voice,Brother Joshua,Victor Aron na Faith Sigers,Safari ameongeza kuwa pia kutakuwepo na maombi ya kumshukuru Mungu kwa kufikisha miaka hamsini ya Uhuru,
Pichani ni baadhi ya waimbaji wa kundi la nyimbo za Injili la Rivers of Live mbele ya Waandishi wa habari (hawapo Pichani),wakiimba akapera mara baada ya kumaliza mkutano wao kuhusiana na tamasha lao litakaloitwa SIFA ZIVUME,la kumsifu na kumuabudu Mungu,tamasha hilo ambalo litaendana sambamba na uzinduzi wa DVD SIFA ZIVUME ambayo ina ujumbe wa kubadili maisha ya watu na kuwapa tumaini,imerekodiwa kwa ubora wa hali ya juu ili kufikia viwango vya Kimataifa,ina urefu wa masaa matatu na inamesheheni nyimbo15

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages