MWENYEKITI WA CCM RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOFUNGUA MKUTANO WA KAMATI KUU YA CCM LEO MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWENYEKITI WA CCM RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPOFUNGUA MKUTANO WA KAMATI KUU YA CCM LEO MJINI DODOMA


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia), akifungua rasmi Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo, ambacho kinatarajia kumalizika kesho. Kutoka kushoto ni Wajumbe wa kudumu wa Kamati Kuu hiyo, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Wajumbe wa Kamati Kuu,  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia), Waziri MKuu, Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofunguliwa na Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete leo, mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakijisomea kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofunguliwa na Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa akisalimiana na Mohamed Dewji, wakati walipokutana ndani ya Ukumbi huo mjini Dodom leo Nevemba 23 wakati wa ufunguzi wa Mkutano  wa Kamati Kuu ya CCM.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Nape Nnauye na Asha Baraka, wakisalimiana wakati walipokutana ndani ya ukumbi huo leo mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, akisalimiana  na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakati walipokutana ndani ya Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mku Mstaafu, Fredrick Sumaye, akisalimiana na Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages