Wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool, ilipokuwa ikiwasili Mkoani Iringa wakati ikiwa safarini kuelekea Malawi, ambapo safari hiyo imeota mbawa na kuwa ni ziara ya mikiani. |
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi
kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI'
yaliyotarajiwa kuanza Novemba 22, hadi 26, 2011.
Akitangaza
mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya
Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya
Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na
chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa
katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa
mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.
Aidha
imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi
kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa
mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali
wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya
Taifa.
Akizungumzia na mtandao huu kuhusu mashindano
hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa. Amos Kafwinga alisema, ”Katika
mashindano ya mwaka huu ya 'ALL AFRICA CUP –MALAWI' yamefutwa kutokana
sababu zilizo nje ya uwezo wa chama cha pool Africa lakini tumefarijika
sana kuona kwamba Bia ya Safari Lager bado iko na sisi bega kwa bega na
kuipa nafasi timu yetu kufanya ziara ya michezo ya kirafiki na timu za
mikoa’’ alisema katibu.
Akitoa
salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa
Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “
Tulipokea taarifa za kufutwa mashindano kwa masigitiko makubwa sana
kwani tulikuwa tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo, lakini
nilifarijika sana kusikia kuwa wadhamini wetu SAFARI LAGER wametupa
nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kutupa michezo ya kirafiki katika mikoa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)