Mkuu
wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Samwel Malechela, akimtunuku Shahada
ya Heshima Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi ,
wakati wa sherehe za Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
yaliyofanyika leo Bungo Kibaha. Kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta
jambo na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Samwel Malechela wakati
wa mahafali hayo ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika
leo Bungo Kibaha.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Mhe. Samweli Malechela, akimtunuku
Shahada ya Udaktari wa Falsafa, Balozi wa Tanzania Nchini Urusi, Balozi
Jaka Mwambi, katika Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
yaliyofanyika leo Bungo Kibaha. kulia ni Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)