Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Bungeni hivi karibuni.
Hatua hiyo inakamilisha mchakato wa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

Rais KIKWETE amesema kuwa Mwananchi yeyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zinazopaswa.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)