Rais
Jakaya Kikwete akimsalimu na kumpa pole mtoto Ali Abdul (13) kutoka
Rufiji, mkoa wa Pwani, aliyetoka kufanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa
ya damu iliyozibwa na madaktari bingwa toka India amabo wako nchini
kusaidia kazi katika kitengo cha tiba ya figo katka Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Kitengo hicho kimeundwa mahususi
kusaidia watu wa matabaka yote kupat matibabu ya figo ikiwa ni moja ya
jitihada za serikali kusaidia wananchi wake kupata matibabu hayo hapa
hapa nchini na kwa gharama nafuu. Rais Kikwete ameonesha kufurahishwa
na kuridhishwa na maendeleo ya kitengo hicho ambacho muda si mrefu
ujao kitakuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa wengi zaidi
Rais
Jakaya Kikwete akiongea na madaktari bingwa toka India wanaosaidia
kazi katika kitengo hicho. Madaktari hao, ambao 16 wanatoka katika
hospitali ya Apollo na wanne toka hospitali ya Madras Mission, wako
nchini kwa ziara ya kikazi ya wiki moja na tayari wamefanya upasuaji
wenye mafanikio wa wagonjwa sita wa figo
Rais
Jakaya Kikwete akiongea na madaktari bingwa wa kutoka India walio
nchini kwa ziara ya kikazi ya wiki moja katika kitengo cha tiba ya figo
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Jumamosi jioni
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wauguzi katika kitengo hicho
Mkuu
wa kitengo na daktari bingwa wa figo, Dk. Linda Ezekiel
akimtambulisha Rais Jakaya Kikwete madaktari bingwa toka India
wanaosaidia kazi katika kitengo cha tiba ya figo katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Rais
Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na madaktari bingwa toka India
na wa Tanzania aliowatembelea katika kitengo cha tiba ya figo katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.Picha Zote na
IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)