HASSAN Shariff Atwaa Ubingwa Wa Mashindano Ya Mbio Za Baiskeli ya (Vodacom Tanzania Tanga Cycle Challenge 2011) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HASSAN Shariff Atwaa Ubingwa Wa Mashindano Ya Mbio Za Baiskeli ya (Vodacom Tanzania Tanga Cycle Challenge 2011)

 Mshindi wa  kwanza  wa Kilomita 140 wa mbio za  baiskeli za “Vodacom Tanga cycle Challenge “  Hassan Sharif akimaliza mbio hizo kwa kwa kutumia masaa 4.13.07 .ambapo mbio hizo zilianzia katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo  hapo jana. 
Washindi wa kwanza na wapili wa mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa kilometa 80 wakimaliza mbio hizo,ambapo Kudushi Nkandi  kushoto aliibuka mshindi na Mohamed Bundala akawa mshindi wa pili.
Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana.
 Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana mjini Tanga ambapo Hassan Sharif aliibuka mshindi kwa kutumia masaa 4:13.07 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja na nusu.
Washiriki mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa walemavu wakimaliza mbio hizo hapo jana mjini Tanga.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa  akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja Mshindi wa kwanza wa mbio za  Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 80,Kadushi Nkandi (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa  akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja  na nusu Mshindi wa kwanza wa mbio za  Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 140,Hassan Sharif (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo kwa kutumia  muda wa masaa 4:13.07 wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu ,afya na uchumi,  Seleboss Mustafa, (kushoto)akimkabidhi  shilingi 75,000.mshindi wa  tatu wa mbio za Vodacom Tanga cycle  Challenge kwa upande wa Kilomita 140 Revocatus Sebastian, aliyetumia  Masaa 4: 15.52 mashindano hayo yaliyoanzia katika uwanja wa Mkwakwani  mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo ,wanaoshuhudia wapili kutoka kushoto ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude,Michael Kasun ambae ni msimamizi wa mawakala wa Vodacom kanda ya Kaskazini.
Mwaandaaji wa Mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge Sophy Wakati akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  kushoto kabla ya mbio hizo kuanza,wa pili kutoka kushoto Buruhani Yakub ambae ni  Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communication na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
---
HASSAN Shariff ametwaa ubingwa wa mashindano ya Mbio za baiskeli ya
(Vodacom Tanga Cycle Challenge 2011)baada ya kumaliza mwendo wa umbali wa kilomita 140 akiwa mbele ya washiriki wengine.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Wakati Sports Promoter na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania  yalishirikisha makundi matatu ambayo ni ya baiskeli zilizotengenezwa maalumu kwa michuano ambapo washiriki walipita Wilaya za Muheza na Korogwe na kurejea Tanga mjini umbali wa kilomita 140.

Sharrif alitwaa ubingwa huo akiwa katika kundi la baiskeli maalumu za mbio hizo ambapo alimaliza michuano hiyo akiwa amekimbia kwa saa 4.13.07 na kufuatiwa na Juma Kashinde aliyetumia muda wa saa 4.14.52 wakati mshindi wa tatu alikuwa Revecatus Sebastian aliyemaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.15.30.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Hamis Milikioni aliyekimbia kwa saa
4.28.08, Mathew Alberto alimaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.35.06 huku Athumani Muya akikimbia kwa saa 4.38.07.

Kundi la baiskeli za kawaida lilianzia Tanga mjini kupitia Tanganyika Wilaya ya Muheza umbali wa kilomita 80 ambapo Kadushi Nkandi aliongoza kwa kutumia muda wa saa 1.56.00,Issa Kashinde alishika nafasi ya pili kwa kumaliza akiwa ametumia muda wa saa 1.57.12 huku Mohamed Bundala alitumia saa 2.15.13.

Baiskeli za miguu mitatu zilikuwa za kulizunguka jiji la Tanga ambapo aliyeongoza ni Jackson Kinyusa aliyekimbia kwa dakika 30.20 akifuatiwa na Mohamed Balozi dakika 32.16 huku Medrin Sabuni akishika ushindi wa tatu kwa kukimbia kwa dakika 45.02.

Mgeni rasmi ,Mohamed Mustapher ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nguvumali na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Tanga,aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuukumbuka mchezo wa baiskeli na kuwaomba kuboresha zaidi mwakani kwani Tanga ni mkoa wenye vipaji vingi.

Mgeni huyo ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Tanga alimkabidhi Shariff kiasi cha sh 150,000, Kashinde sh 100,000,Revocatus sh 75,000 wakati washindi wa kwanza katika makundi ya baiskeli za miguu mitatna za kawaida walizawadiwa sh 100.000,wa pili sh 75,000 wa tatu sh 50,000 huku washiriki wengine wakipewa kifuta jasho cha sh. 10,000 kwa
kila mmoja.

Afisa Udhamini wa Vodacom,Ibrahim Kaunde alisema huu ni mwaka wa pili kwa Kampuni yake kudhamini mashindano ya baiskeli kwa Mkoa wa Tanga na Mwanza lengo likiwa ni kuimarisha mchezo huo katika maeneo hayo kwa kuwa unaonekana kupendwa zaidi.

“Kimsingi Vodacom imejikita kudhamini michuano ya baiskeli Tanga na Mwanza kutokana na ari na mwamko uliopo kama ambavyo tunavyodhamini riadha mkoani Kilimanjaro”alisema Kaunde.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages